Somo la 40: Kuelezea sababu
Tam, Mi Ya na Haru-san wameketi kwenye Nyumba ya Haru-san wakat kitu kisicho cha kawaida kilipotokea.
Jifunze misemo muhimu na kupata ufahamu wa kitamaduni kwa kusikiliza simulizi ya Tam, mwanafunzi wa kimataifa aliyesajiliwa katika chuo kikuu kimoja cha Japani. Shirika la umma la Japani, NHK, linatoa kozi hii ya lugha ya Kijapani kupitia podcast, bila malipo. nhk.jp/lesson
Somo la 40: Kuelezea sababu
Tam, Mi Ya na Haru-san wameketi kwenye Nyumba ya Haru-san wakat kitu kisicho cha kawaida kilipotokea.
Somo la 39: Kuelezea kosa ulilolifanya
Tam ana tatizo! Punde baada ya kurejea kwenye Nyumba ya Haru-san anamwomba Haru-san msaada.
Somo la 38: Kulinganisha vitu viwili
Tam na Ayaka wamepanda usafiri wa majini mahsusi kwa kutalii katika ziwa Ashinoko huko Hakone.
Somo la 37: Kusema kuna tatizo
Inaonekana Tam na Ayaka wana tatizo kwenye chumba chao katika hoteli ya chemchemi ya majimoto huko Hakone.
Somo la 36: Kuulizia saa/muda
Tam na Ayaka wamefika kwenye chemchemi ya majimoto ya Hakone. Mhudumu anawapeleka kwenye chumba chao.
Somo la 35: Kuelezea uliyoyafanya na utakayoyafanya kwa mtiririko
Tam na Ayaka wamo kwenye treni kuelekea Hakone, eneo maarufu la kitalii lililpo jirani na Tokyo.
Somo la 34: Kusema ambacho umewahi kukifanya
Tam na Mike wamefika kwenye "manga café", ambapo kuna mkusanyiko wa vitabu vingi vya katuni za manga pamoja na majarida.
Somo la 33: Kuulizia muda unaohitajika
Kaito na Mike wamefika salama kwenye Makumbusho ya Ninja. Wameamua kujaribu kutumia silaha za ninja za shuriken.
Somo la 32: Kuulizia jinsi ya kufika mahali
Mike na Kaito wanaelekea Makumbusho ya Ninja mkoani Mie. Mike amevalia vazi la ninja.
Somo la 31: Kumwambia mtu mfanye kitu pamoja -- Sehemu 2
Mike, Mmarekani anayependa utamaduni wa Kijapani, amefika kwenye "Nyumba ya Haru-san" kujadili mpango wa safari.
Somo la 30: Kuelezea mambo mbalimbali yaliyopita na yajayo
Tam amefika mgahawani na Mi Ya. Tam anazungumzia kumbukumbu zake kuhusu mwanafunzi wa muziki, Yuuki.
Somo la 29: Kusema ulichokifanya
Mi Ya anamwonesha Tam picha alizopiga kwenye onyesho la kupiga piano Kamakura. Tam anazitazama na kushangazwa.
Somo la 28: Kuomba ruhusa
Mi Ya amefika Kamakura. Maonyesho ya kupiga piano yanafanyika hekaluni.
Somo la 27: Kuulizia kipi cha kuchagua
Kaito amempeleka Tam kwenye mgahawa wa tambi za rameni. Tam anamkumbuka Yuuki, mwanafunzi wa muziki aliyekutana naye Vietnamu.
Somo la 26: Kuelezea fikra zako mbalimbali -- Sehemu 1
Tam na wapangaji wenziwe wamefika kwenye bustani kwa ajili ya kutazama maua ya mcheri.
Somo la 25: Kusema hujihisi vizuri
Tam anaonekana kutojihisi vizuri. Sensa ya Haru-san inabaini tatizo.
Somo la 24: Kuelezea usichoweza kukila
Kwenye Nyumba ya Haru-san, Kaito ametayarisha kifunguakinywa cha kawaida cha Kijapani kwa ajili ya kila mtu.
Somo la 23: Kusema unachopenda
Tam, Ayaka na Mike wamekuja kwenye mgahawa wa paka unakoweza kucheza na paka.
Somo la 22: Kumwambia mtu mfanye kitu pamoja -- Sehemu 1
Tam, Mi Ya na Kaito wapo mbele ya sanamu kubwa ya theluji kwenye tamasha la theluji huko Sapporo.
Somo la 21: Kueleza mahali ulipo
Tam na Mi Ya wapo Hokkaido. Wanakutana na Kaito kwenye Mnara wa Saa wa Sapporo.
Somo la 20: Kumwomba mtu asiweke kitu fulani kwenye chakula chako
Tam na Mi Ya wapo Sapporo, Hokkaido. Wanaingia mgahawani kufurahia chakula cha baharini.
Somo la 19: Kusema unachotaka kununua
Tam anapanga kwenda Hokkaido na Mi Ya na Kaito. Ili kujiandaa kwa safari hiyo, amekuja kununua glavu.
Somo la 18: Kuelezea mvuto wa ulichokifanya
Mi Ya yuko sebuleni kwenye “Nyumba ya Haru-san,” akiwaelezea Tam na mwenyenyumba roboti Haru-san kuhusu safari yake huko Nagano.
Somo la 17: Kuelezea unachokifanya kwa sasa
Mi Ya anapiga picha Nagano. Anakutana na wanandoa wa Kijapani, na wanaenda kwenye mgahawa wa tambi za soba.
Somo la 16: Kuelezea kuvutiwa kwako na kuelezea vitu -- Sehemu 2
Mi Ya yupo katika chemchemi ya majimoto ya mkoani Nagano ambayo ni maarufu kwa nyani wa porini kuoga hapo. Wanandoa wa Kijapani wanaanzisha mazungumzo naye.
Somo la 15: Kumwambia dereva wa teksi mahali unakoelekea
Mi Ya, mpigapicha kutoka China, amefika kwenye mkoa wa Nagano uliopo Japani ili kupiga picha katika chemchemi ya majimoto. Amejaribu kupanda teksi kuelekea kwenye bustani inayoitwa Jigokudani Yaen Koen.
Somo la 14: Kuelezea matamanio yako
Kabla ya kuja Japani, Tam alikuwa mfanyakazi wa kujitolea katika shule ya msingi nchini Vietnamu. Siku moja, Yuuki, mwanafunzi wa shule ya muziki kutoka Japani alifika kuwapigia piano watoto wa shule hiyo.
Somo la 13: Kusema unachotaka kufanya
Tam anazungumza na mwenyenyumba roboti, Haru-san pamoja na Mi Ya mpigapicha katika sebule ya "Nyumba ya Haru-san."
Somo la 12: Kuelezea kuvutiwa kwako na kuelezea vitu -- Sehemu 1
Tam na Mi Ya, mpigapicha kutoka China wapo kwenye Hekalu la Sensoji katika eneo la Asakusa jijini Tokyo. Wapo kwenye sehemu inayouza hirizi.
Somo la 11: Kumuuliza mtu ikiwa ana kitu unachokihitaji
Tam amefika Asakusa jijini Tokyo na Mi Ya, mpigapicha kutoka China. Wawili hao wanazunguka zunguka katika maduka ya zawadi kwenye barabara ya "Nakamise."
Somo la 10: Kuulizia bei ya vitu
Tam, amefika kwenye duka la vifaa vya kielektroniki na rafiki yake Ayaka. Tam anataka kununua kikausha nywele.
Somo la 9: Kuulizia vitu usivyovijua
Tam kutoka Vietnamu amefika kwenye duka la vyakula vilivyo tayari kuliwa lililopo chini ya ardhi kwenye jengo lenye maduka makubwa, linaloitwa "depa-chika," akiwa na Kaito mpangaji mwenzake pamoja na rafiki yake Mmarekani, Mike.
Somo la 8: Kuwatambulisha marafiki kwa wengine
Tam na rafiki yake Ayaka wamekuja kwenye Jengo la Serikali ya Jiji la Tokyo, ambalo hutembelewa na watu ili kuangalia mandhari ya jiji kutokea juu. Wanakutana na Mi Ya.
Somo la 7: Kumwomba mtu azungumze polepole
Tam anakula chakula cha mchana kwenye kafeteria katika chuo kikuu chake. Mwanafunzi wa kike mmoja Mjapani anakuja na kuzungumza naye.
Somo la 6: Kuulizia usafiri wa umma unakoelekea
Ni siku ya kwanza ya Tam kwenda katika chuo kikuu chake. Yupo kwenye kituo cha treni, lakini hana uhakika kama treni hiyo anayotaka kupanda ndiyo sahihi.
Somo la 5: Kusema jinsi ulivyojifunza Kijapani
Ni siku ya kwanza ya masomo katika chuo kikuu kwa Tam. Ana wasiwasi na mwenyenyumba Haru-san ambaye ni roboti anagundua na kuzungumza naye.
Somo la 4: Kusema unachotarajia kufanya
Tam anazungumza na rafiki yake mpya, Mi Ya, mpigapicha kutoka China. Chumba cha Mi Ya kimepambwa kwa picha nyingi kutoka kote nchini Japani.
Somo la 3: Kutaja unakotokea
Karamu ya ukaribisho inafanywa kwa ajili ya Tam, mwanafunzi kutoka Vietnamu, katika nyumba anayoishi. Kaito ameandaa meza iliyosheheni vyakula.
Somo la 2: Kujitambulisha jina na kazi ufanyayo
Tam -mwanafunzi kutoka Vietnamu- anatafuta "Nyumba ya Haru-san." Anakutana na wakazi wa nyumba hiyo ambao wanamwonesha ilipo nyumba hiyo.
Somo la 1: Kuulizia mahali
Tam -mwanafunzi kutoka Vietnamu- anatafuta "Nyumba ya Haru-san". Ni nyumba ya kupanga watu mbalimbali atakayokuwa anaishi akiwa jijini Tokyo.
Con cuenta puedes dejar de 1 a 5 micrófonos. El público ve la media; tu comentario corto lo ves solo tú.
Aún no hay micrófonos. Sé el primero.
Entrar para dejar micrófonos.